Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akivikwa Skafu na Vijana wa UVCCM baada ya kuwasilili Viwanja vya Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Mkata Mashariki Wilaya ya Handeni DC, Mkoa wa Tanga kuhutubia wananchi Septemba 21, 2026.
Na Dotto
Mwaibale, Tanga
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah amesema
kwamba tofauti kubwa iliyopo baina ya CCM na vyama vingine ni wao wanamkataba
na wananchi wa kuwapelekea maendeleo kupitia ilani ya uchaguzi lakini wenzao ni
kutukana matusi kila wanapofanya mikutano yao.
Abdallah ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Mkata Mashariki Wilaya ya Handeni DC, Mkoa wa Tanga ikiwa ni siku ya pili baada ya kuzindua ziara hizo Septemba 19, 2026 Kijiji cha Stahaba kilichopo Kata ya Mikunguni wilayani Pangani.
Alisema
lengo ya chama chochote cha siasa kinaposhiriki uchaguzi ni kushika dola
“CCM inapo shiriki uchaguzi inahakikisha inafanya kila linalowezekana kuwashawishi
wananchi kukiunga mkono na kushika dola,’ alisema.
Alisema
kwenye suala la uchaguzi chama hicho kinakuwa hakina masihara wala mswalie
mtume.
Alisema
katika jambo la kuhakikisha wanashika dola wanatumia busara na hekima
kuwashawishi wananchi wawaunge mkono.
Alisema
wenzao wa vyama vingine wanakuwa hawana mkataba wala hoja zozote zaidi ya kutoa
lugha za matusi kuanzia mwanzo hadi mwisho wa uchaguzi.
Alisema CCM wanapokuwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu
wanakuja na mkataba ulioandaliwa vizuri
kupitia wataalamu wao.
Alisema
mkataba huo ni ilani ya uchaguzi ya CCM na kuwa wanafanya hivyo kila mwaka unapofanyika
uchaguzi.
Rajabu aliongeza kuwa wataalamu hao kazi yao ni kuangalia ahadi zilizotekelezwa na zile ambazo hazikutekelezwa ambapo zinatekelezwa kwenye mwaka mwingine baada ya kuingizwa kwenye ilani ya mwaka husika.
“Tulipofanya
uchaguzi mwaka 2025 utofauti huo ulionekana kwamba CCM inakuja na ilani hiyo
ambayo ndiyo mkataba.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akiwasalimia wananchi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akisisitiza jambo kwenye mmkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akiwa na viongozi wengine wakielekea Uwanja wa mkutano.Vijana wa UVCCM wakiwa tayari kumpokea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akipiga ngoma sambamba na wasanii wakati wa mapokezi yake.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akizindua Shina Namba 16, Kijiwe cha Kange Bodaboda.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akipandisha bendera kuashiria rasmi uzinduzi wa kijiwe hicho.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akizungumza na vijana wa kijiwe hicho baada ya kukizindua.
Wanawake wa UWT ambao ni wajasiriamali wakitoa burudani kabla ya uzinduzi wa kijiwe chao.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah. akicheza na wanawake wa UWT kabla ya kuzindua kijiwe chao.
Taswira ya mkutano wa hadhara uliofanyika Mkata.
Msafara wa magari ukiongozwa na gari la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah kulekea Uwanja wa mkutano.
Viongozi mbalimbali wakiwa wamejipanga foleni wakisubiri kumpokea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akisalimiana na Katibu wa CCM Wilaya ya Tanga, Feruzy Bano wakati wa mapokezi yake.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Burudani zikitolewa
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akishiriki kutoa burudani na wasanii wa kikundi cha Mkata.
Katibu wa CCM Wilaya ya Handeni, Mayasa Kimbau, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Mwanaisha Ulenge, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Tanga, Samwel Mngazija, akizungumza kwenye mkatano huo.
Naibu Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Khalid Hamza, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Tanga ni Hassan Ramadhani Mbezi, akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, akizungumza kwenye mkutano huo.
Vijana wa Hamasa wakiziteka nyoyo za wananchi kwa burudani safi.


0 Comments